Katika Hili, VIJANA Wengi Wa Kitanzania Bado Wako Gizani.

Internet ni mfumo mkubwa sana wa kompyuta unaounganisha mamilioni ya kompyuta ulimwenguni pote. Ili kujua ukubwa wake,Inktomi, kampuni inayotayarisha programu za kompyuta, ilitumia muda wa miezi minne kuchunguza na kuainisha Web. Ilipata nini? Idadi ya kurasa zisizo za kawaida ilikuwa zaidi ya bilioni moja! Kiingereza ndicho kilichokuwa lugha inayotumiwa zaidi katika Internet. Hutumiwa zaidi ya mara asilimia 86 ya wakati wote. Zaidi ya asilimia 2 tu ya hati zote zilizo katika Internet ni za Kifaransa, nacho Kiholanzi kilikuwa asilimia 0.5.

Kulingana na kampuni ya Google, mamilioni ya tovuti huongezwa kwenye Intaneti kila siku. —NEW SCIENTIST, UINGEREZA.

Siku hizi mtu anaweza kutumia Intaneti mahali popote kama vile katika maduka yenye huduma za Intaneti (Internet café), akiwa ofisini, kwenye simu za mkononi na vifaa vingine kama hivyo. 

Fikiria baadhi ya mambo ambayo watu wanafanya kwenye Intaneti na hatari na uzuri wake.

BARUA PEPE

Ni nini? Ni ujumbe ulioandikwa unaotumwa kupitia kompyuta.

Kwa nini inavutia? Barua pepe ni njia ya haraka na isiyo ghali ya kuwasiliana na marafiki na watu wa familia.

Unachopaswa kujua. Mbali na kuudhi, barua usizotaka zinaweza kuwa na madhara. Mara nyingi zina habari zinazogusia au kutaja moja kwa moja mambo machafu. Anwani nyingine za ziada zinaweza kumwomba mtumiaji, kutia ndani mtu asiyejua, atoe habari za binafsi ambazo zinaweza kufanya utambulisho wake uibiwe. Kujibu barua hizo, hata ikiwa unatuma ujumbe unaosema usitumiwe barua hizo, kutathibitisha kwamba anwani hiyo inatumiwa, na hilo linaweza kufanya utumiwe barua zaidi.

TOVUTI

Ni nini? Ni kurasa za kompyuta ambazo zimetengenezwa na mashirika, taasisi za elimu, biashara, na watu mmoja-mmoja.

Kwa nini zinavutia? Kuna mamilioni ya tovuti zinazowawezesha watu kununua vitu, kufanya utafiti, kuwasiliana na marafiki, na kucheza au kunakili michezo na muziki.

Unachopaswa kujua. Tovuti zimetumiwa vibaya na watu wasio na nia nzuri. Vituo vingi vinaonyesha watu wakifanya ngono, na ni rahisi kwa watu wasio makini kuvifungua bila kukusudia. Kwa mfano, nchini Marekani uchunguzi uliofanyiwa vijana walio kati ya umri wa miaka 8 na 16 ulionyesha kwamba asilimia 90 ya vijana hao walipata bila kukusudia ponografia (picha au habari za ngono) kwenye Intaneti, mara nyingi walipokuwa wakifanya kazi za shule! Jambo la kupendeza ni kwamba, nyingi ya tovuti za ngono zimepigwa marufuku mtandaoni.

Lakini pia hebu angalia takwimu za wale wanaotumia intaneti kwa manufaa mazuri ya familia na ustawi wa jamii zao… 

“Asilimia 1 ya watu matajiri zaidi ulimwenguni wanamiliki asilimia 40 ya utajiri ulio kwenye sayari hii,” linasema gazeti la London Guardian. “Wale wanaoshughulikia huduma za kifedha na Intaneti ni kati ya watu matajiri zaidi,” linasema gazeti hilo. Utafiti mmoja uliofanywa na Umoja wa Mataifa ulionyesha kwamba asilimia 37 ya watu matajiri zaidi wanaishi Marekani, asilimia 27 Japani na asilimia 6 wanaishi Uingereza. Asilimia 50 ya watu maskini duniani wanamiliki chini ya asilimia 1 ya utajiri duniani. Kulingana na Duncan Green, ambaye ni mkuu wa utafiti katika Oxfam nchini Uingereza, “kiwango hicho cha matajiri wanajihusisha na intaneti. . . . Haiwezekani kutoa sababu nzuri ya watu wachache kuwa na utajiri mwingi hivyo huku watu milioni 800 wanalala njaa kila siku.”

Makala Zinazofanana na Hii:

JAMBO LA KUPENDEZA: Unaweza kujifunza namna ya kunufaika na teknolojia na hasa matumizi ya mitandao ya kijamii ukaanza kunufaika.

VITUO VYA MAONGEZI

Ni nini? Ni vituo fulani kwenye Intaneti ambavyo watu wanaweza kuwa na mazungumzo ya wakati uleule kupitia kuandikiana kuhusu habari fulani.

Kwa nini vinavutia? Unaweza kuwasiliana na watu wengi walio na mapendezi sawa ambao huenda hujawahi kukutana nao.

Unachopaswa kujua. Mara nyingi, watu wanapendelea kuwasiliana na watu wanaofahamiana nao na ikiwezekana kuonana nao wakati huo huo. Lakini pia, waajiri wengi sasa wanapendelea kutumia njia hii kuwasahili watu walioomba kazi kwenye makampuni/mashirika yao. Mfano wa vituo hivi ni Skype, Immo n.k

UJUMBE MFUPI

Ni nini? Ni mawasiliano ya moja kwa moja kati ya watu wawili au zaidi kupitia ujumbe ulioandikwa.

Kwa nini unavutia? Njia hii ya mawasiliano humwezesha mtu kuchagua marafiki atakaowasiliana nao walio katika orodha yake. Hivyo, haishangazi kwamba uchunguzi uliofanywa nchini Kanada unaripoti kwamba asilimia 84 ya vijana walio na umri wa kati ya miaka 16 na 17 wanawatumia marafiki wao ujumbe mfupi na wao hufanya hivyo kwa zaidi ya saa moja kila siku. Nchini Tanzania, kwa takwimu za hivi karibuni… inakisiwa watu zaidi ya milioni 18 wanatumia WhatsApp, Telegram n.k kuwasiliana kwa ujumbe mfupi wa maneno, picha, sauti, video n.k

Unachopaswa kujua. Ujumbe mfupi unaweza kukengeusha mtu ikiwa anapaswa kufanya jambo linalohitaji awe makini. Kwa kuongezea, unaweza kuanza kutengeneza hela kutoka kwa watu unaowasiliana nao kila siku kupitia ujumbe mfupi endapo ukiamua kujiunga na programu ya mafunzo yetu sasa.

BLOGU

Ni nini? Ni vitabu vya kuandika mambo ya kibinafsi kwenye Intaneti.

Kwa nini zinavutia? Blogu huwapa watu nafasi ya kuandika mawazo yao, mapendezi na mambo wanayofanya. Blogu nyingi zinawaruhusu wasomaji waandike maelezo yao na watoto wengi wanafurahi wanapopata kwamba mtu fulani ameandika maelezo yake.

Unachopaswa kujua. Habari zilizo kwenye blogu zinaweza kusomwa na mtu yeyote. Baadhi ya vijana hutoa bila kujali habari zinazoweza kutumiwa kutambulisha familia yao, shule, au mahali wanapoishi. Pia, blogu zinaweza kutumiwa kuchafua majina ya watu, kutia ndani kumharibia sifa mwenye blogu hiyo. Kwa mfano, baadhi ya waajiri hufungua blogu ya mtu aliyeomba kazi wanapochunguza ikiwa wanaweza kumwajiri mtu huyo.

Habari Njema. Vijana wengi wanajiingizia kipato kikubwa kwa siku, wiki na hata kwa mwezi kwa kutumia blogu zao. Hata hivyo, sipendekezi mtindo unaotumiwa na wana-blogu wengi wa hapa Tanzania. Zipo njia nyingine nzuri unazoweza kupata hela pasina kutegemea matangazo, AdSense na njia nyingine zilizo zoeleka. Tunatoa mafunzo ya njia nzuri mbala wa zinazotumika sasa.

MITANDAO YA KIJAMII

Ni nini? Ni vituo ambavyo vinawaruhusu watu watengeneze tovuti zao na kuziboresha kwa kutumia picha, video, na blogu.

Kwa nini vinavutia? Kuanzisha na kuboresha kituo chake kunamwezesha mtu ajitambulishe. Mitandao ya kijamii inawaruhusu watu kukutana na “marafiki” wengi wapya.

Unachopaswa kujua. Mtandao wa kijamii ni kama sherehe kwenye Intaneti.  Watu wenye nia mbaya wanaweza kuwasiliana nawe. Habari za kibinafsi zinazowekwa kwenye vituo vya mawasiliano zinaweza kutumiwa vibaya na vijana na watu wazima wenye nia mbaya. 

Zaidi ya hilo, urafiki kwenye Intaneti kwa muda mrefu umekuwa ni wa kijuu-juu tu. Watu hudiriki kuwakubalia urafiki watu ambao hawajakutana nao uso kwa uso ili waonekane kuwa maarufu na watu wanaotembelea kurasa zao. Katika kitabu chake Generation MySpace, Candice Kelsey anaandika kwamba “ubora wa mtu unaamuliwa na idadi ya watu wanaompenda.”

Anaongeza hivi:

[penci_blockquote style=”style-1″ align=”none” author=”Candice Kelsey”]“Kuamua ubora wa mtu kupitia idadi ya watu wanaompenda na kumfuata kunawafanya wafanyabiashara kumtafuta muhusika hili awatangazie bidhaa/huduma zao kupitia ukurasa wake. Jambo hilo limewasababisha vijana wengine wengi wakose utu na kunawashinikiza sana wajitambulishe kwa njia itakayowaletea marafiki wengi zaidi hili nao wapate matangazo kupitia kurasa zao. [/penci_blockquote]

Kwa hiyo, kitabu What in the World Are Youth Doing Online? kinatoa mapendekezo haya muhimu:

“Vijana yafaa wajifunze namna bora ya kuweza kujiingizia kipato kupitia mitandao ya kijamii pasina kuvunja heshima na hata kuingilia faragha ya watu wengine?”

Mifano hiyo sita ni baadhi ya mambo yanayowavutia watu kutumia Intaneti. Ikiwa wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kujifunza namna ya matumizi ya intaneti yenye manufaa, unaweza… 

Nitumie Ujumbe


Nitumie Ujumbe

Leave a Reply