An apple a day keeps the doctor away

Address:

227 Marion Street, Columbia, SC 29201

Awamu 4 Anazopitia Mfanyabiashara wa Soko la Mtandao Kuelekea Mafanikio

Awamu nne ninazoenda kuangazia katika makala haya zitakusaidia kujitathimini mahali ulipo na kukupa mwangaza wa kukuandaa kisaikolojia juu ya safari uliyoianza ama unayotaka kuanza. Lengo kubwa ni kukidhi haja yako ya kupata mafanikio unayokusudia.

Katika makala hii nitazungumza na network marketer, affiliate marketer na blogger. Lakini zaidi nalenga kumsaidia yule anayefikiria kuanza biashara hizi kwa sababu tu, kamwona fulani amefanikiwa au kaambiwa kuwa biashara hizi zinalipa.

NDIYO zinalipa… ila SI katika njia rahisi kama inavyosemekana.

Hebu tuanze kwa kuangazia juu ya dhana ambayo nimeona inawasumbua watu wengi… dhana ya MATARAJIO!

Matarajio ni kila kitu, sivyo?

Lakini hebu fikiria hii:

**********************************************

Umekutana na rafiki yako Suzi mnayeheshimiana sana akiwa na kijana fulani hivi mwenye mvuto. Rose anakuomba kumtambulisha kwako rafiki yake John anayefanya kazi katika moja ya ofisi ambayo umekuwa ukitamani siku moja ufanyie kazi. Anamwelezea John jinsi alivyo mchapakazi, mweledi, mwelevu, makini na kubwa zaidi – ambavyo yeye Rose ujihisi mwenye furaha sana awapo karibu naye. Anaenda mbali zaidi na kummiminia sifa nyingi kuhusu jinsi John alivyo na vipawa vingi vya kushangaza na vya ajabu.

Ki-kawaida… utakuwa na shauku ya kukutana naye… sivyo? 🙂

(Namaanisha, amemfanya aonekane mtu muhimu sana ambaye unadhani makutano yenu yanaweza yakawa chanzo cha wewe kutimiza ndoto baadi ya zako).

Baada ya utambulisho, mnasalimiana na John na kisha mnabadilishana mawasiliano na mnapanga kukutana kwa ajili ya mazungumzo 😉

Mara, siku inawadia ambayo mlipanga kukutana kupata kinywaji kwenye moja ya hoteli iliyo karibu na mtaa unaoishi. Unachukua muda wa ziada kujiandaa ili nawe uonekane vyema ukizingatia namna John alivyo pasina kusahau jinsi Suzi alivyomtambulisha.

Hupendi kubaki nyuma 🙂

Ili usichelewe, unaamua upande Uber…

Baada ya kushuka kwenye Uber unajiandaa kuingia kwenye hoteli, mara unamwona John yuleee kasimama karibu na mlango.

Ukiwa umejawa na hofu kiasi… mara anakukaribisha huku mkitembea taratibu kuelekea bar.

Baada ya kuagiza kinywaji na kuanza mazungumza kwa dakika 10 hivi, unagundua jambo… (Sawa, ana mwonekano mzuri na anaonekana kuwa na uwezo wa kutosha)

Lakini unagundua kwamba hana tofauti na wanaume wengine ambao umewahi kukutana nao kabla. Hapendi kazi yake. Anapenda kuangalia sinema za hovyo, muziki, soka na zaidi ya yote… kashaanza kuelewa. Baada ya muda kidogo, anaanza kuimba na ghafla anaanza kusinzia sababu ya ulevi 🙁

Hivi, utajisikiaje?

Kwa kiasi fulani, utahisi kukata tamaa zaidi kwa sababu umetumia muda wako mwingi kujiandaa ukijua unaenda kukutana na mtu muhimu sana lakini kumbe unaenda kukutana na mtu wa hovyo.

Ni kama vile umekutana na copy ya mtu fulani hivi…

Sasa swali la kujiuliza ni Je, ni wa hovyo kweli? Je, kuna jambo lolote baya juu yake?

Jibu ni HAPANA.

Tatizo ni wewe… yaani MATARAJIO yako!

Uliweka matarajio ya juu zaidi kuliko ukweli wenyewe na hivyo kukufanya kukata tamaa na kuhisi kuumia zaidi.

*************************************

Sasa hebu tuondokane na scenario hiyo na turudi katika uhalisia…

Wote kwa nyakati tofauti, tumekuwa tukikutana na hali za namna hii katika nyanja tofauti tofauti. Kama kwako bado… kawaulize wanandoa, wahitimu wa vyuo n.k. Watakueleza nini yalikuwa mataraji yao kabla ya ndoa au kabla ya kumaliza vyuo…

Au nenda kahudhurie semina za biashara ya soko la mtandao. Mmmh, si kwa pesa zile utakazoonyeshwa… 😉 Endapo unashindwa kuzuia hisia zako basi siku hiyo utajiunga au utakosa usingizi kama hukuwa na hela ya kuanza. Najua wengi mnanielewa!

Tunakutana sana na mambo haya katika maisha. Hebu fikiria sinema…. bongo movie.

Unapoangalia aina fulani ya filamu nzuri, unadhani kwamba maisha yako hivyo.

Huwa ninawaangalia sana watu wanaoendeshwa na hisia au matarajio kwa sababu ya kaona au kaambiwa jambo fulani!

Kwa sababu hiyo, nikitaka kupendekeza jambo fulani… ujitahidi kuwa makini ili kuepukana na kumjengea mtu matarajio! Mara nyingi nikitaka kupendekeza aiona fulani ya biashara utasikia nikisema…

…Ikiwa hujaona ama kusikia biashara hii, basi ITAKUCHANGANYA! Naomba ichunguze kwa umakini kama nilivyofanya kwa sababu imezidi sana matarajio yangu!

Analojia hii ya MATARAJIO inaweza kuonekana ya kawaida – lakini husababisha matatizo makubwa kwa watu na hasa wafanyabiashara wapya.

Ni kawaida kuwasikia wakiwa  na matarajio makubwa, jambo ambalo SI baya hata kidogo, ila huwa napata wasi wasi pale ninaposikia mtu akisema: “Ninachohitaji kufanya ni kuandika makala chache na kuziunganisha na bidhaa na kuanza kuingiza maelfu ya dola…” 🙁 Au nitakuwa na-post biadhaa zangu kwenye mitandao ya kijamii na kisha kupata wateja.

SI Sawa.

Mtu wa namna hiyo, baada ya muda wa miezi kadhaa (asipofikia matarajio yake) mara utaanza kusikia maneno haya wakati wote:

 • Kwa nini mimi bado sijatengeneza pesa?
 • Network Marketing ni ngumu!
 • Huwezi kutengeneza pesa mtandaoni!
 • WordPress ni ngumu sana?
 • Mara Oooh, mimi nimetamaushwa na X, Y, Z!
 • Blog hazifanyi kazi, n.k.

Ukisikia mtu anatoa kauli hizo, kuna sababu muhimu. Naam, labda sababu mbili muhimu…

 1. Alidanganywa mara kadhaa, aliambiwa kuwa jambo hili ama lile ni rahisi…
 2. Alikuwa na matarajio yaliyozidi kiasi kuhusu mafanikio yatokanayo na jambo husika.

Kwa sababu hiyo, nataka kutolea ufafanuzi zaidi juu ya safari ya mafanikio katika biashara hizi zilivyo zaidi ya inavyosemekana.

Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifanya utafiti kutia ndani uzoefu na uelewa wangu juu ya biashara na hatimaye nikaja na matokeo ambayo sehemu yake itaelezwa katika makala hii.

Leo nitazungumzia juu ya awamu nne kama sehemu ya utafiti wangu.

Huu hapa apa ni muhtasari:

AWAMU YA 1: HOVYO
AWAMU YA 2: KIGOLI
AWAMU YA 3: ROKETI
AWAMU YA 4: UKOMO

Muhtasari wa nilichojifunza…

Karibu katika kila jambo ambalo unaenda kufanikiwa, daima halitakuwa katika unyoofu. Mara nyingi utapoteza hela, muda na kuanguka. Bibi yangu alikuwa na kawaida ya kuniambia kwamba “Muda na hela zinazopotea bure huwa ni nyingi kuliko zile zilizotumika kuleta tija, suala la msingi ni kutokukata tamaa hasa unapokuwa na hakika na kile unachofanya.”

Sasa hebu tuangazie awamu ya kwanza

HOVYO

Ikiwa utaniuliza sababu #1 kwa nini watu wanashindwa kupata ufanisi katika maisha, hilo ndo litakuwa jibu langu. Kwa sababu mwanzoni mwa safari yoyote na katika kujifunza jambo lolote kuna changamoto nyingi ambazo daima uhumiza.

Hawamu hii napenda kuiita HOVYO.

Kama blogger na mmiliki wa biashara mtandaoni, kuna wakati ninapofanya kazi ngumu na hata kutumia pesa nyingi bila kwenda mahali popote. Kuna wakati ninajihisi kama mtu unayejaribu kusukuma ukuta mkubwa wa matofali, kupitia theluji, kuelekea mlima Everest, au sawa na mbwa nayejaribu kung’ata mkia wake.

Kwanini Hili Utokea? Kuna Sababu Kadhaa…

Kubwa kuliko zote ni kwamba huna ujuzi wowote. Ujuzi huja baada ya kuwekeza muda, jitihada, na pengine kujitoa sadaka. Safari ya Ujasiriamali ni mchezo mwingine kabisa. Pengine, ndiyo maana asilimia kubwa ukimbilia katafuta ajira wakisahahu kwamba wanaenda kuajiriwa na wajasirimali ambao hawakuogopa changamoto wanazokimbia wao.

Na kwa sababu huna ujuzi, kila kitu unachofanya mwanzoni ni hovyo kabisa.

 1. Machapisho yako katika blogu ni ya hovyo, kwa sababu…
 2. Jinsi unavyowasilisha biashara yako ni namna ya hovyo pengine kwa sababu…
 3. Mawazo yako ni ya hovyo.

Na kuna uwezekano mkubwa, kwa wakati fulani… utaanza kujihisi wa hovyo.

Pia, hii ni sababu mojawapo ambayo huifanya awamu hii kuwa vigumu sana kuivuka: Ni…

Awamu inayokupasa uwekeze NGUVU na JITIHADA nyingi sana na wakati huo hauna chochote cha kuonyesha.

Kumbe, unajikuta sio tu kwamba haupati matokeo yoyote… bali pia unaifanya hiyo biashara ionekane ya hovyo machoni pa watu.

Ngoja niwe mkweli katika hili…

Asilimia 96% ya watu wanaoanza wakiwa HAWANA KITU hupata changamoto kuvuka awamu hii, na hivyo wengi wao huishia njiani.

Hivi hujakutana na watu wanaoisema vibaya biashara ya network marketing? Kwani unadhani sababu ni nini? Wanakatisha tamaa hao 🙁 Usiombe kukutana nao… watakueleza sababu millioni moja za jinsi ambavyo network marketing haifai.

Kama umeshakautana nao, au ukimsikia mtu anayesema vibaya biashara hizi basi ujue kwamba hakuwa na guts za kuvuka awamu ya kwanza na hivyo aliishia hapo.

ANGALIZO!
Siko hapa kukukatisha tamaa na wala kuiburudisha akili na hisia zako kwa kuipaka sukari ili biashara hii ionekane rahisi kama wafanyavyo wengine… HAPANA. Niko hapa kukueleza ukweli ili wakati unapofika… basi ufanye maamuzi yaliyo sahihi.

Nalazimika kutoa tahadhari hii kwa maana baadhi ya watu (hasa wafanyabishara wa soko la mtandao – Network Marketing – wasio waaminifu) hunishambulia vikali kwamba napotosha watu.

Baada ya kutoa angalizo hilo, napenda kusisitiza tena hapa kwamba…  biashara hii siyo rahisi hata kidogo! Kama unadhani hivyo, UNAKOSEA.

Napenda kujitenga na watu wasiopenda kueleza ukweli.

Lakini mbaya zaidi ni jamii yetu… inawafundisha watu kuepuka maumivu. Wanasahau kwamba jambo lolote ambalo linakufanya ujihisi vizuri sasajambo hilo hilo lilikufanya ujihisi VIBAYA hapo kabla.

Kiukweli, jamii yetu na hasa ya kizazi cha nyakati hizi cha iGen inapenda kupata vitu kiulaini kama wanavyotafuna jojo au kulamba ice-cream. Jamii yetu ina kawaida ya kutumia lugha mbaya ambayo pengine huwafanya watu kupoteza mwelekeo wa ndoto zao.

USHAURI WANGU…

Jitenge na watu wenye mtizamo hasi juu ya wazo lako. Kaa nao mbali sana… hata kama ni wazazi wako. Usisahau kwamba hii ni karne ya 21… dunia iliyowakuza wao si dunia unayoishi wewe.

Ikiwa unataka kuvuka awamu hii, kuna mambo mawili tu unayopaswa kuzingatia;

 1. Usikate tamaa.
 2. Endelea kusonga mbele.

Kadri siku zitakavyosonga mbele, ndivyo mambo yatakavyoendelea kuachia taratibu. Yataenda hatua kwa hatua. Jambo muhimu ni kuzidi kujifunza mbinu mpya huku ukirekebisha makosa ya mwanzo… amini kwamba ipo nuru mbele hata kama bado upo katikati ya shimo la giza. Nuru ipo!

Awamu hii inaweza ikakuchua miaka 5, miezi 5, au siku 5. Hivyo ndivyo ilivyo vigumu sana kuhusu hilo. Mambo huwa tofauti kwa kila mtu, ikizingatiwa kwamba kila mtu anayo njia yake.

Kuna mambo mengi ambayo yanaingia ndani yake, ikiwa ni pamoja na muda unaowekeza, jinsi unavyozingatia mafunzo, mafanikio uliyonayo hapo kabla, n.k.

Jambo la kuzingatiwa.

Kila mtu aliyefanikiwa, alipitia hii hatua ambayo binafsi napenda kuiita awamu ya hovyo.

Ni sawa na ibada ya mfungo na hiyo inakuweka mbali na wengine.

Endapo utazingatia hilo, ukajifunza na kufundishika, ukaweka akili wazi, ukasikiliza, ukaweka bidii ya kazi, na kuendelea kukua… UTATOKA tu.

Taratibu utaanza kuona mabadiliko katika biashara zako na hatimaye pesa kuanza kutiririka na hapo ndipo unapoanza kuingia katika awamu inayofuata… yaani awamu ya 2:

KIGOLI

Kwa wasiojua, KIGOLI ni binti aliye katika umri wa kubalehe. Binti anayekuwa katika kipindi cha mabadiliko ya mwili kuelekea utu uzima.

Mara nakupenda, mara anakuchukia. Mara ni moto, mara ni baridi tena barafu. Wakati huo huo utasikia analia akiwa bafuni kwa sababu rafiki yake alikuwa amevaa mavazi sawa na yeye kanisani na hivyo anadhani maisha yake sasa YAMEKWISHA. Baadaye kidogo… utamsikia akipiga kelele kufurahia jambo na mpezi wake katika simu akimweleza juu ya mwanamziki mpya anayempenda.

Yeye ni roller-coaster wa kihisia ambayo inafafanua awamu ya pili.

Karibu kwenye awamu ya kigoli.

Hiki ni kipindi cha turbulence ya kihisia za juu na chini ambazo huanza mara moja baada ya kuanza kunasa wateja kama sumaku. Mara tu unapoanza kutengeneza kipato chako cha mwanzo… unafurahi kweli kweli, mara unaanza kujiambia “Nimeweza! Niko sahihi! Niko mwamba! Nimeweza kutambua jambo hili! ”

Samahani… HUSIJIDANGANYE.

Natumaini ungefundwa kwa undani juu ya awamu hii kwa sababu hivi ndivyo jinsi biashara yako itakavyo kuwa:

 • Mauzo yatakuwa mazuri siku ya kwanza na huenda hayatakuwapo siku ya pili.
 • Chapisho lako au tangazo laweza kuvumishiwa ukajikuta tovuti yako inafungwa kwa sababu ya tatizo la kiufundi ambalo hukulitegemea.
 • Utafikiria unajua kila kitu na kuwa na uthibitisho usiofaa katika jambo ambalo hamna, na kujikuta ukijiuliza maswali ya kile ulichodhani unajua.
 • Utapata hamasa kubwa sana (kwa sababu mafanikio hatimaye hukufanya ujihisi ndo wewe) kumbe inakurudisha kwenye shimo la moto (maovu huanza kuibuka baada ya kuonja mafanikio).

Unakuwa chini mara juu, na juu mara chini. Hali hii inatokea kwa sababu ni mzunguko wa kihisia.

Unautulizaje?

Itategemeana na jinsi wewe mwenyewe unavyoweza kukabiliana na hisia mbovu… hizi zinaweza kuwa siku ngumu zaidi.

Unapokuwa katika awamu ya HOVYO, unakuwa na tabia ya kunyonya. Faida yake ni kwamba matarajio yanakuwa ni ya chini.

Awamu ya KIGOLI uhumiza zaidi. Ni sawa na mtu anayenyatia kutokea nyuma na ghafla kukushtua. Ukifanya kosa tu ukageuka… KIGOLI inachukua kila kitu kutoka kwako.

Ngoja nikupe mfano mwingine… Ni sawa na rafiki wa kike ambaye mmekutana baa. Anachopenda kwako ni bear na vipande vya pesa kwa dakika mtakazokubaliana. Akishakupa mgongo ukamuita tena, hakujui… inabidi mzungumze biashara upya 🙂

Hiyo ndo awamu ya pili… KIGOLI.

Sifa yake nyingine ni kwamba, inaweza kudumu kwa muda mrefu kwa baadhi na wengine haichukui muda.

Chukua hatua hizi zifuatazo uweze kuepukana nayo:

1. Jifunze jinsi ya kuwa wa kawaida.

Tofauti na kawaida, utajihisi kila wakati unakuwa na mkazo wa kihisia ukiwaza mauzo ya mwezi ujao na hata kushindwa. Kadri unavyoweza kusimamia hisia zako, ndivyo unaweza kushinda mikazo hiyo. Hapo hakuna kufanyiwa maombi, lazima ujifunze namna ya kukabiliana na hisia. Jifunze kuwa wa kawaida… ukipata pesa nyingi na hata ukipata kidogo. Kuwa wa kawaida.

2. Ongeza kiwango cha mkondo wa mapato.

Hisia za kuchanganyikiwa pale unapo poteza biashara au kazi huwa hazimtawali mtu mwenye kuwa na vyanzo mbalimbali vya mapato. Mwezi mbaya wa mauzo kwenye biashara moja hautakuathiri sana kama una baishara nyingine kumi. Ni mchanganuo rahisi.

3. Boresha mahusiano yako na wateja wako.

Kadri unavyoboresha zaidi mahusiano na watu, husabababisha hata wasiokujua kuanza kununua bidhaa na hata kujiunga na biashara yako. Kuna njia elfu za kuboresha uhusiano na kwa kadri utakavyozidi kugundua siri, ndivyo utakavyozidi kupunguza msongo wa mawazo…. Niamini.

Hatua ya mwisho inaonekana kuchanganya lakini inawezekana.

Awamu ya 3:

ROKETI

Hii ndio hatua pendwa ambayo kila mmoja huitumainia katika safari yake. Pengine ndiyo maana unafanya kazi kwa bidii sana na kujitoa sadaka mwanzoni ili uweze kufikia hataua hii.

Mara baada ya mifumo thabiti kuwako, jambo pekee unalozingatia ni KUKUZA BIASHARA.

Ni katika awamu hii mambo hufurahisha na kushangiliwa… unaanza kujulikana na kupata heshima kwa sababu…

Kufika awamu hii unakuwa unafahamu “siri” na umepitia mambo mengi na ndiyo maana mtu aliyefika hapa hufanya mchakato uonekane rahisi.

Wote waliofikia hatua hii, mara utawaona wamepakia picha kwenye mitandao ya kijamii wakiwa katika hoteli kubwa kubwa, wanaendesha magari mazuri, na wakati mwingine wako beach wamepakata laptop zao.

Roketi, kwa sababu ya uzito wake, hutumia nguvu kubwa sana kabla haijaanza kuruka kuelekea juu. Huchukua muda mwingi aridhini huku ikiunguza mafuta mengi zaidi na uhitaji nguvu kubwa sana kuweza kunyanyuka.

Hata hivyo, kwa kadri inavyotumia nguvu sana kuweza kuruka, ikisha shika hatamu huko angani, nguvu ndogo huhitajika kuweza kuiongoza.

Hivyo ndivo ilivyo hata katika biashara.

Mara baada ya mambo kuanza kwenda vizuri, utastaajabishwa na jinsi nguvu kidogo inayohitajika kuweza kuchochea biashara iende. Hebu fikiria unapokuwa unapanda mlima Kilimanjaro inakuwaje? Mwanzoni huwa ni maumivu katika kupanda na inahitaji kiasi kikubwa cha damu, jasho, na machozi, lakini mambo yanaweza kuwa rahisi kwa kadri unavyoendelea.

Na hii si kwa sababu kuna uchawi unametokea, la hasha. Ni kwa sababu umepata ujuzi wa aina mbalimbali wakati wa awamu mbili za mwanzo, na ujuzi huu una athari nyingi kwa wakati huo. Kwa mkutadha huu nitatolea mifano zaidi kwa watu wanaofanya biashara ya Affiliate Marketing ambayo binafsi nafanya. Wengi wao utakuta wanajipatia hela nyingi kupitia katika kuuza kozi zitakazokusaidia ku-save muda…

Huongoza taratibu zote.
Affiliate Marketer mara baada ya kujenga ukurasa mmoja wa mauzo, awamu ya pili itaenda haraka zaidi. Hali hiyo inakwenda na kila kipengele cha blogu kiufundi. Kwa sababu wanauzoefu tayari…

Wanakupa ufahamu zaidi unaohitaji kujua ni nini kinachofuatia.
Bado utafanya makosa, lakini mbinu za zamani ulizojifunza zinaondoka kwenye soko na na hivyo unahitaji kujifunza mbinu mpya. Mfano kujua kuwa unachukia tovuti zinazokuhitaji ujisajili inatokana na ukweli kwamba pengine ulionywa kwamba husitoe taarifa zako kwa tovuti usizofahamu fika wamiliki wake. Huo ni mtizamo wa kizamani. Elimu siku hizi inasambazwa kwa njia ya email pamoja na mitandao ya kijamii, hivyo ni vyema sana kuwa na mwelekeo wa jumla ulionao.

Wanasaidia kuzuia kupoteza muda.
Kwa sababu mwanzoni, utakuwa ukipoteza masaa mengi kwa mambo ambayo siyo. Ikiwa hutaki, basi hafanyii mazoezi kwa bidii.

Inakupasa kujifunza jinsi ya kuandika makala za blogu kwa haraka na kwa ufanisi zenye kichwa cha habari ambacho kitanasa macho na hisia za watu. Unajua nini cha kufanya wakati kitu kikiharibika. Unajua jinsi ya kushughulika na kila tatizo au huduma kwa wateja na kujiandaa kuwa tayari kwa chochote.

Stadi hizi pia ni muhimu kwa usalama wa biashara yako. Binafsi, ninaweza kuanzisha blogu ikafanikiwa sana ikiwa nitataka kwa sababu sasa ninao ujuzi na mbinu mbali mbali za kufanya hivyo..

Kwa sababu unakuwa umepata stadi hizi zote wakati wa mchakato wa awamu zilizotangulia, kila kitu huenda kwa haraka sana kiasi kwamba unahisi kama unaweza kufika mbali na kutumia muda mwingi kufurahi.

Na kisha kuna awamu moja ya mwisho …

Awamu ya 4:

UKOMO

Japo bado sijafikia awamu hii, lakini ninajua sana kwamba ipo inakuja.

Kuna kikomo kwa watu wangapi ambao wanavutiwa na blogu duniani na kwamwe kuna ukomo wa ukuaji wa biashara yoyote ile.

Bila kuacha kufanya mambo ambayo unatakiwa kufanya, awamu ya ukomo ipo tu.

Ni imani yangu binafsi kwamba madhumuni ya kila biashara si kuwepo milele na milele.

Hitaji hili la ukuaji wa mara kwa mara husababisha makampuni na wamiliki wa biashara kufanya maamuzi yasiyo ya kimaadili na kupoteza mwelekeo wa wateja wao wa awali.

Angalia kwenye Facebook.

Mfano mzuri ni Facebook, kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo pia inavyozidi kupoteza mvuto miongoni mwa watumiaji wake kwa sababu imekuwa ikihitaji faida zaidi na zaidi ili kukidhi wanahisa.

Hii hutokea kwa kila kampuni.

Ukweli ni kwamba biashara yako itakuwa na wateja kwa kiwango fulani ambao kimsingi ndo walengwa na lengo lako ni kufika pale. Ukisha fika hapo, hakikisha unalinda maadili na shikilia hapo.

Hii ina maana gani? Usipende kukua haraka haraka kisa tu unakua. Ikiwa una kitu kizuri kinachoendelea shikilia ngome na uendelee.

Hii pia haimaanishi kuwa ni vibaya kukua haraka, la hasha. Nachomanisha ni kwamba endelea kusikiliza wateja wako ulionao, boresha na kubadilisha biashara yako kulingana na mahitaji ya wakati.

Kwa makadirio yangu, ikiwa nitajitahidi sana kupitia blogu hii, ninaweza kuingiza kati ya 50M – 100M kwa mwezi. Kuchukua hatua yoyote zaidi itahitaji mkakati mpya wa masoko, timu kubwa zaidi, na si tu kukaa chini.

Ikiwa unataka vitu hivi, endelea kuviendea hadi uvifikie. Binafsi nataka ziada ya kipato kutoka katika biashara zangu.

Tambua kwamba kila biashara itafikia hatua hii. Awamu ya UKOMO.

Kwa wengine, itawawia vigumu na wengine rahisi, kulingana na kiasi gani ulivyojipanga.

Hivyo ndivyo zilivyo awamu za mafanikio katika biashara unazoona. Daima ni busara kufanya hesabu zako kabla ya kuwa na haja ya kubadilisha mkakati wako wa masoko na kutafuta timu ya kukusaidia.

Leave a Comment

(0 Comments)

Your email address will not be published. Required fields are marked *

shares