Awamu 4 za Mafanikio ya Mwanablogu

Awamu nne ninazoenda kuangazia katika makala haya zitakusaidia kujitathimini mahali ulipo na kutoa mwangaza wa ni-hatua gani zichukuliwe. Lengo likiwa ni kuifanya blogu yako ikidhi matakwa yako ya kukuingizia kipato.

Hapa nazungumza na blogger wa aina yoyote ile. Lakini zaidi naenda kumsaidia yule anayefikiria kuanzisha blogu kwa sababu tu, kamwona fulani amefanikiwa au kaambiwa kuwa na blogu kunalipa.

NDYO inalipa… lakini endapo utazingitia mambo kadhaa kutia ndani haya manne nitakayokueleza hapa na mengine mengi ninayofundisha kupitia darasa hili maalum.

Hebu tuanze kwa kuangazia juu ya dhana hii ambayo nimeona inawasumbua watu wengi… dhana ya MATARAJIO!

Matarajio ni kila kitu, sivyo?

Lakini hebu fikiria hii: Rafiki yako Suzi anakutambulisha kwa boss wake wa moja ya ofisi ambayo unatamani siku moja ufanyie kazi. Anamwelezea boss wake huyo kwa jinsi alivyo vizuri, mchapakazi, mwenye akili, makini, na muhimu zaidi – ujihisi mwenye furaha sana awapo karibu naye. Anaendelea mbele zaidi kwa kummiminia sifa nyingi kuhusu jinsi boss wake huyo alivyo na vipawa vingi vya kushangaza na vya ajabu.

Ki-kawaida, utafurahi kukutana naye.

Namaanisha, amemfanya aonekane kama mtu muhimu sana ambaye makutano yenu yanaweza yakawa chanzo cha kutimiza ndoto zako nyingi…

Unasalimiana na boss wake huyo na kubadilishana mawasiliano na unamwomba kukutana naye 😉

Hatimaye, siku yenyewe inafika ambayo mlipanga kukutana kupata kinywaji kwenye moja ya bar mtaani. Unachukua muda wa ziada kujiandaa ili nawe uonekane vyema ukizingatia namna yeye alivyo kwa mujibu wa kile ulichoelezwa na rafiki yako. Nawe hupendi kubaki nyuma.

Ili usichelewe, unaamua upande Uber… Unaposhuka na kutaka kuingia katika baa, unagundua jamaa kasimama karibu na mlango.

Ukiwa umejawa na hofu kiasi… mara anakukaribisha huku mkitembea taratibu kuelekea ndani.

Baada ya kukaa na kuzungumza naye kwa dakika 10 hivi, unagundua jambo.

Namaanisha, sawa ana mwonekano mzuri… na anaonekana kuwa na uwezo wa kutosha, lakini hana tofauti na wanaume wengine ambao umewahi kukutana nao kabla. Hapendi kazi yake. Anapenda kuangalia sinema za ngono, muziki, soka na tayari kashaanza kuelewa. Baada ya muda kidogo, anaanza kuimba sababu ya ulevi na kucheza muziki 🙂

Kwa kiasi fulani, unajisikia kukata tamaa zaidi kwa sababu umetumia muda wako mwingi kujiandaa ukijua unaenda kukutana na mtu muhimu sana lakini kinyume chake unakutana na mtu wa kushangaza.

Ni kama vile umekutana na copy ya mtu fulani.

Siyo kwamba kuna jambo lolote baya juu yake. La hasha.

Tatizo ni MATARAJIO yako… yalikuwa ya juu zaidi kuliko ukweli wenyewe na hivyo kukufanya kukata tamaa na kuumizwa zaidi.

Wote tumekuwa tukikutana na hali za namna hii. Kama bado, waulize wanandoa, wahitimu wa vyuo n.k. Watakueleza…

Au nenda kahudhurie semina za biashara ya mtandao. Si kwa cheki zile… 😉 Endapo unashindwa kuzuia hisia zako basi siku hiyo utakosa usingizi…

Unapoangalia aina fulani ya filamu nzuri, unadhani kwamba maisha yatakuwa hivyo. Mpenzi wako akiwa anapendezwa na jambo hili au lile nawe unadhani kwa kuwa anapendezwa nalo basi jambo hilo ni zuri sana. …au kama anachukizwa na jambo fulani, basi nawe unachukizwa nalo. Na hasa endapo matarajio yako yalikuwa chini, basi anazidi kukuchanganya.

Huwa ninawaangalia sana… Watu wanaoendeshwa na hisia au matarajio kwa sababu ya fulani!

Kwa sababu hiyo, nikitaka kupendekeza jambo fulani…hujitahidi kuwa makini ili kuepukana na kukujengea matarajio! Mara nyingi utasikia nikisema…

…Ikiwa ujaona ama kusikia biashara hii bado, ITAKUCHANGANYA! (Nataka uiangalie kwa umakini kama nilivyofanya, kwa sababu imezidi sana matarajio yangu!)

Analojia hii ya MATARAJIO inaweza kuonekana ya kawaida – lakini husababisha matatizo makubwa kwa watu na hata bloggers wapya.

Ni kawaida kuwasikia bloggers wakiwa  na matarajio makubwa, jambo ambalo SI baya hata kidogo, bali huwa napata wasi wasi pale ninaposikia mtu akisema: “Ninachohitaji kufanya ni kuandika makala chache na kuziunganisha na bidhaa na nitaweza kuingiza maelfu ya dola, sawa!?”

Si sawa.

Baada ya muda wa miezi kadhaa (asipofikia matarajio yake) unaanza kusikia maneno kama haya wakati wote:

  • Kwa nini mimi bado sijatengeneza pesa?
  • WordPress ni ngumu sana?
  • Mara Oooh, mimi nimetamaushwa na X, Y, Z!

 

Wakati watu wanatoa kauli hizo, kuna sababu muhimu. Naam, labda sababu mbili muhimu…

Walikuwa wakidanganywa mara nyingi sana kama watoto, wakiambiwa kuwa jambo hili ama lile ni rahisi sana…

Imepelekea pia matarajio mabaya kuhusu mafanikio yatokanayo na blogu.

Kwa sababu hii, nataka kutolea ufafanuzi zaidi juu ya safari ya blogging ilivyo zaidi ya inavyosemekana.

Kwa vidokezo vingi vya bure vya blogu na tricks kutoka kwangu, hakikisha kujiunga na DARASA letu!

Hapa ni muhtasari wa awamu ambazo tutaziangazia:

AWAMU YA 1: HOVYO
AWAMU YA 2: KIGOLI
AWAMU YA 3: ROKETI
AWAMU YA 4: UKOMO

Nini nimejifunza kutika safari yangu ya biashara hizi za mtandao…

Mafanikio, karibu katika kila kitu ambacho nimekuwa na mafanikio katika maisha yangu daima hayakuwa katika unyoofu. Nimepoteza hela mara nyingi na kuanguka. Anguko likiwa la mtaani na mtandaoni. Lakini, bado sijakata tamaa na wala sifikirii kukata tamaa.

Sasa hebu tuangazie…

Awamu ya 1: HOVYO

Ikiwa utaniuliza sababu # 1 kwa nini watu wanashindwa kupata ufanisi katika maisha hii ndiyo sababu.

Kwa sababu mwanzoni mwa safari yoyote, kujifunza jambo lolote, huwa ni changamoto. Daima uhumiza.

Hawamu hii napenda kuiita HOVYO.

Kama blogger na mmiliki wa biashara mtandaoni, kuna wakati unapofanya kazi ngumu na hata kutumia pesa nyingi bila kwenda mahali popote. Unaweza kujihisi kama unajaribu kusukuma ukuta mkubwa wa matofali, kupitia theluji, kuelekea mlima Everest.

Kuna sababu ya hili kutokea.

Huna ujuzi wowote bado [katika ulimwengu wa mtandaoni]. Ujuzi huja baada ya muda, jitihada, na kujitoa sadaka. Biashara za mtandaoni ni mchezo mwingine kabisa.

Na kwa sababu huna ujuzi, kila kitu unachofanya mwanzoni ni hovyo kabisa.

  • Machapisho yako katika blogu ni ya hovyo.
  • Mawazo yako ni ya hovyo.
  • Namna unavyo wasilisha bidhaa yako ni katika namna ya hovyo.
  • Na kuna uwezekano mkubwa, kwa wakati fulani, utaanza kujihisi wa hovyo.

Hii ni sababu mojawapo ambayo huifanya awamu hii kuwa vigumu sana kuivuka:

Ni awamu ambayo inakupasa uwekeze NGUVU na JITIHADA nyingi sana na wakati huo hauna chochote cha kuonyesha. Hivyo, sio tu haupati matokeo yoyote, bali pia unaifanya hiyo biashara ionekane ya hovyo.

Asilimia 99% ya watu wanaoanza wakiwa HAWANA KITU hupata changamoto kuvuka awamu hii. Kwa sababu ni ngumu.

Kumbuka:

Siko hapa kuiburudisha akili na hisia zako wala kupaka sukari hizi biashara zionekane rahisi kama wafanyavyo wengine… HAPANA. Niko hapa kukueleza ukweli ili unapotaka kufanya maamuzi ya kufanya biashara hizi, basi ufanye maamuzi yaliyo sahihi.

Naendelea kusisitiza hapa… Sio rahisi hata kidogo! Kama unadhani hivyo, UNAKOSEA.

Na mbaya zaidi ni jamii yetu… inawafundisha watu kuepuka maumivu. Wanasahau kwamba jambo lolote ambalo linakufanya ujihisi vizuri jambo hilo lilikufanya ujihisi VIBAYA hapo kabla.

Kiukweli, jamii yetu na hasa ya nyakati hizi inapenda kupata vitu kiulaini kama walivyozoea kutafuna jojo na kulamba ice-cream. Hutumia lugha mbaya kuwafanya watu kupoteza mwelekeo wa mawazo yao.

Jitenge na watu wenye mtizamo hasi juu ya wazo lako. Kaa nao mbali hasa, hata kama ni wazazi wako. Dunia iliyowakuza wao si dunia unayoishi wewe.

Ikiwa unataka kuvuka awamu hii, kuna mambo mawili tu unayopaswa kufanya …

  1. Usikate tamaa.
  2. Endelea kusonga mbele.

Kadri siku zitakavyosonga mbele, ndivyo mambo yatakavyo endelea kuachia taratibu, itakuwa ni hatua kwa hatua. Jambo muhimu ni kuendelea mbele ukijifunza mbinu mpya, ukirekebisha makosa ya mwanzo huku ukijua wazi kwamba ipo nuru mbele hata kama bado upo katikati ya shimo la giza.

Awamu hii inaweza kuisha baada ya miaka 5, miezi 5, au siku 5. Hivyo ndivyo ilivyo vigumu sana kuhusu hilo. Mambo huwa tofauti kwa kila mtu, ikizingatiwa kwamba kila mtu anayo njia yake.

Kuna mambo mengi ambayo yanaingia ndani yake, ikiwa ni pamoja na muda unaowekeza, jinsi ulivyozingatia mafunzo, jinsi ya mafanikio uliyonayo, n.k.

Hapa kuna jambo la kuzingatiwa.

Kila mtu aliyefanikiwa, alipitia hii ambayo binafsi napenda kuiita awamu ya hovyo. Ni sawa na ibada ya mfungo na hiyo inakuweka mbali na wengine.

Endapo utazingatia hilo, ukajifunza na kufundishika, ukaweka akili wazi, ukasikiliza, ukaweka bidii ya kazi, na kuendelea kukua… UTATOKA tu.

Taratibu utaanza kuona mabadiliko katika biashara zako na hatimaye pesa kuanza kutiririka… hapo ndipo unapoanza kuingia katika awamu inayofuata…

Awamu ya 2: Kigoli

Anakupenda – anakuchukia. Mara ni moto – mara ni baridi (barafu). Wakati mmoja yeye analia akiwa bafuni juu ya jinsi rafiki yake alivyokuwa amevaa sawa na yeye shuleni na maisha yake sasa YAMEKWISHA, baadaye utamsikia akipiga kelele kufurahia jambo na mpezi wake katika simu akimweleza juu ya mwanamziki mpya anayempenda.

Yeye ni rollercoaster wa kihisia ambayo inafafanua awamu ya pili ya kuwa na aina yoyote ya biashara.

 

Karibu kwenye awamu ya kigoli.

Hiki ni kipindi cha turbulence ya kihisia za juu na chini ambazo huanza mara moja baada ya kuanza kupata attraction. Mara tu unapoanza kutengeneza kipato chako cha kwanza kupitia intaneti, mara unaanza kujidanganya “Nimeweza! Niko sahihi! Niko mwamba! Nimeweza kutambua jambo hili! ”

Samahani, HUSIJIDANGANYE.

Natumaini umefundwa ndani ya awamu hii kwa sababu hivi ndivyo jinsi biashara yako itaenda:

Mauzo yatakuwa mazuri siku ya kwanza na huenda hayatakuwapo siku ya pili.

Chapisho lako au tangazo laweza kuvumishiwa ukajikuta tovuti yako inafungwa kwa sababu ya suala la kiufundi.

Utafikiria unajua kitu na kuwa na uthibitisho usiofaa katika jambo ambalo hamna, na kujikuta ukijiuliza maswali ya kile ulichofikiri unajua.

Utapata hamasa kubwa sana (kwa sababu mafanikio hatimaye hukufanya ujihisi ndo wewe) kumbe inakurudisha kwenye shimo la moto (maovu huanza kuibuka baada ya kuonja mafanikio).

Unakuwa chini mara juu, na juu mara chini. Itakuja kuwa mzunguko wa kihisia.

Kulingana na jinsi wewe mwenyewe utakavyoweza kukabiliana na msongo wa mawazo, hizi zinaweza kuwa siku ngumu zaidi.

Unapokuwa katika awamu ya HOVYO, kiasi unakuwa na matarajio ya kunyonya. Au angalau unapaswa. Faida ya mwanzo ni kwamba matarajio yanakuwa ni ya chini.

Hata hivyo, awamu ya KIGOLI ni mojawapo ambayo huumiza zaidi kama inakupa matumaini tu na kukushtua kutokea nyuma ili ukifanya kosa ukageuka tu, inachukua kila kitu kutoka kwako.

Ni kama kuwa na rafiki wa kike ambaye mmekutana baa. Anachopenda kwako ni bear na hivyo vipande vya pesa kwa dakika mtakazokubaliana. Mkishamalizana, ukikutana baada ya dakika, hakujui tena.

Awamu hii inaweza kudumu kwa muda mrefu kwa watu na wengine kamwe hawawezi kuiepuka. Ikiwa uko katika awamu hii, chukua hatua hizi zifuatazo:

Jifunze jinsi ya kuwa wa kawaida.

Isipokuwa labda michakato yako ni ya kawaida, utajihisi kila wakati umefungwa kihisia na mafanikio ya mwezi ujao na kushindwa. Kadri unavyoweza kusimamia hisia zako, ndivyo unavyoshinda mikazo hiyo na kwa kasi unaweza kushinda. Hapo hakuna maombi, lazima ujifunze namna ya kukabiliana na hisia.

Ongeza kiwango cha mikondo ya kipato.
Hisia za kuchanganyikiwa pale unapo poteza biashara au kazi huwa hazimtawali mtu mwenye kuwa na vyanzo mbalimbali vya mapato. Mwezi mbaya wa mauzo kwenye bidhaa moja hauathiri sana kama bidhaa nyingine kumi. Mchanganuo rahisi.

Kuboresha mchakato wako.
Kadri unavyoboresha zaidi mahusiano na watu, husabababisha hata wasiokujua kuanza kununua moja ya bidhaa zako. Kuna njia elfu za kuboresha mchakato huu na kwa kadri unavyogundua siri, ndivyo unavyozidi kupunguza msongo wa mawazo. Niamini.

Awamu ya mwisho ni weird kwa sababu inaonekana kama fantasy lakini mpaka uifikie.

Awamu ya 3: Roketi

Hii ndio maana unafanya kazi kwa bidii sana na kujitoa sadaka mwanzoni.

Mara baada ya mifumo yako kuwako, jambo pekee unalozingatia ni KUKUZA BIASHARA.

Na ndipo mahala ambapo mambo hufurahisha…

Kufika katika awamu hii ni “siri” nyuma ya kwa nini bloggers wengine na hata wana masoko wengi hufanya kila kitu kionekane rahisi. Hii ni kwa nini wanaweza kupiga picha wakiwa beach wamepakata laptop zao.

Roketi, kwa sababu ya uzito wake, kutumia nguvu kubwa sana kuruka juu. Huchukua muda mwingi aridhini huku ikiunguza mafuta zaidi na uhitaji nguvu kubwa sana kuweza kunyanyuka.

Hata hivyo, kwa kadri inavyotumia nguvu sana kuweza kuruka, ikisha shika hatamu huko angani, nguvu ndogo huhitajika kuweza kuiongoza.

Biashara za mtandaoni si tofauti sana.

Mara baada ya mambo kuanza kwenda vizuri, utastaajabishwa na jinsi nguvu kidogo inayohitajika kuweza kuchochea biashara iende. Mwanzoni huwa ni maumivu katika kupanda na inahitaji kiasi kikubwa cha damu, jasho, na machozi, lakini mambo yanaweza kuwa rahisi kwa kadri unavyoendelea.

Na hii si kwa sababu ya kitu fulani cha kichawi kinachotokea, la hasha. Ni kwa sababu umepata ujuzi wa aina mbalimbali wakati wa awamu mbili za kwanza, na ujuzi huu una athari nyingi kwa wakati wako:

Wao huongeza taratibu zote.
Mara baada ya kujenga ukurasa mmoja wa mauzo, awamu ya pili itaenda haraka zaidi. Hali hiyo inakwenda na kila kipengele cha blogu kiufundi.

Wanakupa ufahamu zaidi unaohitaji kujua ni nini kinachofuatia.
Bado utafanya makosa, lakini masomo ya zamani uliyojifunza yanaondoka kwenye soko na na hivyo unahitaji kujifunza mbinu mpya. Vitu kama kujua kuwa unachukia tovuti zinazokuhitaji ujisajili itatokana naukweli kwamba kutoka kwenye uzoefu ni vyema sana kwa mwelekeo wa jumla unapaswa kuwa nao.

Wanasaidia kuzuia kupoteza muda.
Kwa sababu mwanzoni, utakuwa ukipoteza masaa mengi kwa mambo ambayo siyo. Ikiwa hutaki, basi hafanyii mazoezi kwa bidii.

Unajua jinsi ya kufanya chapisho la blogu kwa haraka na kwa ufanisi lenye kichwa cha habari ambacho kitakamata macho na hisia za watu. Unajua nini cha kufanya wakati kitu kikiharibika. Ulishughulika na kila tatizo la huduma kwa wateja kwa mtu na tayari kwa chochote.

Stadi hizi pia ni kwa nini kuna usalama mkubwa katika biashara hii. Binafsi, ninaweza kuanzisha blogu ikafanikiwa sana ikiwa nitataka kwa sababu sasa ninao ujuzi na mbinu mbali mbali za kufanya hivyo..

Kwa sababu umepata stadi hizi zote kwenye mchakato, kila kitu huenda kwa haraka sana kiasi kwamba unahisi kama unaweza kufika mbali na kutumia muda mwingi tu kufurahi.

Na kisha kuna awamu moja ya mwisho …

Awamu ya 4: Ukomo

Japo kwa sasa bado sijafikia awamu hii, lakini ninajua sana kwamba iko.

Kuna kikomo kwa watu wangapi ambao wanavutiwa na blogu duniani na kuna kikomo kwa ukuaji wa biashara YOTE.

Bila kuacha na kufanya mambo ambayo hutaki kufanya, hata hivyo. Ipo tu.

Ni imani yangu binafsi kwamba madhumuni ya kila biashara haipaswi kuendelezwa ukuaji wa milele na milele.

Hitaji hili la ukuaji wa mara kwa mara husababisha makampuni na wamiliki wa biashara kufanya maamuzi yasiyo ya kimaadili na kupoteza mwelekeo wa wateja wao wa awali.

Angalia kwenye Facebook.

Jukwaa lao linazidi kuwa baya zaidi kila mwaka kwa sababu inahitaji faida zaidi na zaidi ili kukidhi wanahisa. Hadi sasa ambapo uzoefu wa jumla wa mtumiaji ni uharibifu.

Hii hutokea kwa kila kampuni.

Ukweli ni kwamba biashara yako mtandaoni itakuwa na wasikilizaji wachache ambao ni walengwa na lengo lako ni kufika pale, huku ukiweka maadili yako, na kaa huko.

Nini maana yake ni hii. Usipende kukua zaidi kwa ajili ya kukua. Ikiwa una kitu kizuri kinachoendelea, shikilia ngome na uendelee.

Hii pia haimaanishi kuwa ni vibaya kukua na hivyo uamue kuficha kichwa chako ndani ya shimo, la hasha. Endelea kusikiliza wateja wako hao, boresha na kubadilisha biashara yako kulingana na mahitaji ya wakati.

Kwa makadirio yangu, ikiwa nitajitahidi sana kupitia blogu hii, nitawaeza kuingiza kati ya 20M – 40M kwa kila mwezi. Kuchukua hatua yoyote zaidi itahitaji mkakati mpya wa masoko, timu kubwa zaidi, na si tu kukaa chini.

Ikiwa unataka vitu hivi, unaendelea kuviendea hadi uvifikie. Binafsi nataka ziada ya kipato kutoka katika biashara zangu.

Tambua kwamba kila biashara itafikia alama hii.

Kwa wengine, itakuwa juu au chini, kulingana na kiasi gani unataka kuiingiza.

Lakini ndivyo mafanikio ya mtandaoni yanavyoonekana. Daima ni busara kufanya hesabu zako kabla ya kuwa na haja ya kubadilisha mkakati wako wa masoko na kukodisha timu kukusaidia.

Leave a Reply